Shati la Ali limechakaa. Anahitaji jingine jipya.
アリのシャツはぼろぼろになってきた。新しいのが必要だ。
Anaenda madukani kununua nguo mpya.
彼は新しい服を探しにショッピングモールにやって来た。
Akiwa madukani, haoni duka la nguo.
ショッピングモールに服屋が見当たらない。
Anaenda dukani kuulizia uelekeo. “Wapi ninaweza kununua nguo?” Anauliza.
だれかに聞いてみようと思い、店に入って「服屋はどこですか」とたずねた。
Muuzaji anaonyesha upande wa pili wa maduka. Duka la nguo lipo upande wa pili.
店の主人はモールの向かい側を指した。服屋は反対側にあったのだ!
Ali anaingia na kuangalia mashati. Mashati ni makubwa mno kwake na ni ghali sana.
アリは店に入って、シャツを探した。だがシャツはどれも大きすぎる。値段もかなり高い。
Badala yake, ananunua suruali mpya kwa sababu zinauzwa. Anaamua kwamba atanunua shati mwezi ujao atakapopata mshahara wake.
代わりに、新しいズボンを買うことにした。セールになっていたからだ。シャツは来月の給料が出てから買うことに決めた。