“Baridi imeshaanza siku hizi. Hivi joto likoje?”
「だんだん寒くなってきましたね。気温は何度ですか?」
“Ni nyuzijoto tisa. Bado ni majira ya kupukutika kwa majani lakini kipupwe kinakaribia.”
「9度です。今はまだ秋ですが、もうすぐ冬ですね」
“Ninasubiria majira ya kuchipua lakini ninapenda majira ya joto, kukiwa vizuri na kuna joto.”
「春が待ち遠しいです。でも私は、暖かくて過ごしやすい夏の方が好きです」
“Sina shida na baridi. Ni mvua na upepo ndiyo sipendi.”
「私は寒さは気になりませんが、雨と風が好きではありません」
“Tazama wingu jeusi. Kesho mvua itanyesha. Kutakuwa na upepo pia. Huenda kutakuwa na dhoruba.”
「あの暗い雲を見てください。明日は雨が降って、風も強くなりそうです。おそらく嵐になるでしょう」
“Bora isiwe hivyo. Kiukweli sipendi hali ya hewa mbaya, hususani ngurumo na radi. Ninaogopa nisije nikapigwa na radi.”
「そうならないといいですね。悪天候、特に雷が本当に好きではありません。雷が落ちてくるかもしれないと思うと怖いんです」