Mai anatafuta filamu ya kutazama. Anataka kwenda kwenye sinema na rafiki yake kipenzi, Lisa.
Mai cerca un film da vedere. Vuole andare al cinema con la sua migliore amica, Lisa.
Mai anapanda skuta yake kwenda kwenye sinema. Wamekubaliana kukutana huko.
Mai prende lo scooter per andare al cinema. Hanno deciso di incontrarsi lì.
Huko kwenye sinema wanasalimiana. Wana shauku ya kutazama filamu.
Al cinema si salutano. Non vedono l’ora di vedere il film.
Mai ananunua tiketi za wote wawili katika kaunta ya tiketi.
Mai compra i biglietti per tutte e due al botteghino.
Pia ananunua popkorni nyingi.
Compra anche un bel po’ di popcorn.
Lisa anabeba popkorni wakati Mai ananunua chupa mbili za soda.
Lisa prende il popcorn mentre Mai compra due bottiglie di soda.
Wanaonesha tiketi zao kabla ya kuingia ndani kutazama filamu.
Mostrano i biglietti prima di entrare nella sala a vedere il film.
Wanatafuta viti vyao. Kuna giza kwa sababu filamu tayari imeanza.
Cercano i loro posti al buio perché il film è già iniziato.
Wanakaa chini ili watazame filamu.
Si siedono a guardare il film.
Ni filamu ya mapenzi, ambayo ndiyo wanayoipenda zaidi.
È un film romantico. È il loro genere preferito.
Baada ya filamu wanaagana na kwenda nyumbani.
Dopo il film si salutano e tornano a casa.