Ladda ner PDF
Tillbaka till listan med berättelser

Mume mzee

Skriven av Aranya

Illustrerad av Sunniva Høiby-Øiset

Översatt av Jacob Haule

Uppläst av Idrisa Mbaraka

Språk swahili

Nivå Nivå 5

Läs hela berättelsen

Reading speed

Automatisk avspälning


Nilifikiri wanaume wa Norwei ni wanaume bora duniani, lakini hii si kweli! Kabla sijaonana na mwanaume ambaye alikuja kuwa mume wangu, nilikuwa ninafanya kazi kiwandani Bangkok na yeye aliishi Pattaya. Tulikutana mtandaoni na hatimaye tukawa wapenzi.


Baada ya muda tukaamua kuoana. Ninatoka katika familia maskini, kwa hiyo kuwa na mume kutoka nchi nyingine ambaye atahudumia familia yangu ilikuwa ni miongoni mwa sababu za kuolewa nae.


Tulihamia Norwei na nilianza kwenda shule kujifunza Kinorwei. Ulikuwa ni wakati mgumu sana. Sikuwa na leseni ya udereva na mume wangu akawa ananipeleka shuleni, ananisubiri na ananirudisha nyumbani. Ilikuwa ni umbali wa saa moja. Baada ya muda, tulihamia karibu lakini alisisitiza kuendelea kunipeleka shuleni. Hakutaka nitembee peke yangu.


Sikuwahi kuwa na pesa tangu nihamie Norwei. Mara moja, mume wangu alinipa pesa kwa ajili ya chakula cha mchana lakini kwa sababu ni pesa kidogo, niliweka kando. Rafiki zangu shuleni walitaka kunisaidia nipate kazi lakini mume wangu alisema haiwezekani. Hafikirii kama kufanya kazi ya usafi ni kazi inayokubalika kwangu.


Badala yake, alinitafutia kazi nyingine, kujenga gereji. Alikuwa bosi na nilifanya kila kitu. Alikuwa hawezi kufanya makubwa kwa sababu alikuwa mgonjwa. Hakuwahi kunipa pesa aliyoipata kutokana na kazi ya kujenga gereji.


Siku moja alisema kuwa anahisi upweke akiwa peke yake nyumbani. Kwa hiyo, tuliamua kuwa na mbwa. Sikutaka mbwa kwa sababu nilikuwa nimechoka baada ya kutoka shule na nilikuwa na kazi nilizopewa nizifanye nyumbani. Alisema ataweza kumtembeza mbwa kila siku lakini mwishowe nililazimika kuwahudumia wote, mbwa na mume wangu mzee.


Sielewi hata itakuwaje, mpango wangu ni kwenda shule nyingine lakini mume wangu hapendi nifanye hivyo. Ana mpango wa kuniongezea ugumu. Ninataka kupinga lakini sijui nafanyaje, si rahisi kuishi katika nchi ya ugenini na mume mzee kama nilivyofikiri.


Skriven av: Aranya
Illustrerad av: Sunniva Høiby-Øiset
Översatt av: Jacob Haule
Uppläst av: Idrisa Mbaraka
Språk: swahili
Nivå: Nivå 5
Creative Commons Licens
Detta verk är licensierat under en Creative Commons Erkännande 4.0 Internationell Licens.
Valmöjligheter
Tillbaka till listan med berättelser Ladda ner PDF