Edson alizaliwa Angola baada tu ya nchi hiyo kupata uhuru. Alikuwa ni mvulana mrefu sana. Kwa sababu ya kimo chake, alikuwa anaonekana sana. Watu waliokuwa wanawapa watoto silaha ili wapigane kama wanajeshi katika vita ya wenyewe kwa wenyewe, walipenda wavulana kama yeye.
Mama yake alikuwa na hofu kwamba wangemteka. Kwa hiyo, aliamua kumpeleka Ureno na shangazi yake. Alidhani angekuwa salama huko.
Kwanza lilikuwa ni jambo gumu sana, kwani Edson alikumbuka hali ya hewa yenye joto, chakula cha asili, na zaidi ya yote, kumbatio la mama yake na mabusu.
Hakuwa anazungumza Kireno vizuri na ilimwia vigumu kumudu masomo yake pamoja na mawasiliano na wanafunzi wenzake. Kwa ujumla, alianza kuhisi kama haukua uamuzi mzuri kwenda Ureno.
Siku moja, mwalimu alibaini jinsi alivyokuwa mizuri katika mpira wa kikapu. Alijiunga na timu ya mpira wa kikapu na alikuwa na mafanikio makubwa. Alipata umaarufu shuleni na alijitengenezea marafiki. Pia alijiamini zaidi.
Kwa kuwa sasa ni mtu mzima, Edson anawafundisha watoto wa wakimbizi na wale walio katika hatari ya kutengwa na jamii. Mwanzoni, kimo chake kilimuweka katika hatari ya kuwa askari mtoto. Sasa, kimo chake kinampa nguvu ya kusaidia wengine ili nao wajihisi wako salama.