“Una familia yoyote?”
“Do you have any family?”
“Ndiyo, mimi na mume wangu tuna mabinti wawili na mtoto wa kiume.”
“Yes, my husband and I have two daughters and a son.”
“Mimi pia nina mabinti wawili lakini nimeachika.”
“I also have two daughters, but I’m divorced.”
“Mabinti zako wana umri gani?”
“How old are your daughters?”
“Mina ana miaka minne. Anasoma darasa la awali. Miriam ana miaka kumi, kwa hiyo, anasoma shule ya msingi.”
“Mina is four years old. She goes to preschool. Miriam is ten, so she goes to school.”
“Watoto wangu wote wanasoma. Mtoto wangu wa kiume atahitimu mwakani.”
“All of my children are in school. My son will graduate next year.”
“Vizuri sana! Wanakua haraka. Anataka kufanya nini baada ya hapo?”
“That is great! They grow up so fast. What does he want to do afterwards?”
“Anataka apate kazi lakini badala yake ninamshauri aende chuo kikuu.”
“He wants to get a job, but I tell him he should go to university instead.”
“Ni wazo zuri. Ninatumaini pia siku moja wanangu wataenda chuo kikuu.”
“That’s a good idea. I also hope my children will go to university someday.”