Kwanza, anafagia sakafu kwa kutumia ufagio.
First, he sweeps the floor with a broom.
Kisha anasafisha kwa kifyonza vumbi. Kifyonza vumbi kinafanya kazi vizuri.
Then he vacuums. The vacuum cleaner works well.
Kisha anachukua ndoo ya maji na deki.
Then he gets a bucket of water and a mop.
Anatupa takataka kwenye pipa la taka na anaweka mfuko mpya ndani yake.
He empties the bin and puts a new bag in it.
Anatupa takataka nje.
He takes out the rubbish.
Anahitaji glavu, sponji na kiowevu cha kusafishia.
He needs gloves, a sponge, and some cleaner.
Anasugua eneo chafu sakafuni kwa kutumia sponji na kiowevu cha kusafishia.
He scrubs a dirty spot on the floor with the sponge and some of the cleaner.
Kisha anasafisha dirisha.
Then he cleans the window.
Sebule yake haiko sawa kabisa.
His living room is very messy.
Anapanga vitu juu. Sasa iko vizuri na safi.
He tidies up. Now it is nice and clean.