Alamu inalia. Ni wakati wa kuamka.
The alarm rings. It is time to get up.
Anaenda bafuni.
She goes to the bathroom.
Anaoga na kisha anaosha nywele zake.
She takes a shower and washes her hair.
Anajifuta maji kwa kutumia taulo.
She dries herself with a towel.
Anavaa nguo. Anavaa sketi na blauzi.
She gets dressed. She puts on a skirt and a blouse.
Anachukua mkoba wake.
She picks up her handbag.
Anabeba mkoba wake na kwenda kazini.
She takes her handbag and leaves for work.
Anatembea kwa miguu kwenda kazini.
She walks to work.
Anafika kazini na kuanza kufanya kazi ofisini.
She arrives at work. She works in an office.