Carlos anaendesha skuta. Anaendesha kwa kasi.
Carlos rides a scooter. He rides fast.
Kuna maji barabarani. Barabara ina utelezi.
There is water on the road. The road is slippery.
Skuta inamshinda na anaanguka.
He loses control of the scooter and falls off.
Mwanamke anapiga simu kuwaita ambulensi. “Ajali imetokea. Njooni haraka!”
A woman calls for an ambulance. “There has been an accident. Come quickly!”
Ambulensi inafika haraka sana.
The ambulance comes very quickly.
Wanaume wawili wanamweka Carlos kwenye machela.
Two men put Carlos on a stretcher.
Wanampakia Carlos kwenye ambulensi.
They lift Carlos into the ambulance.
Ambulensi inaelekea hospitalini.
The ambulance drives to the hospital.
Nesi anamuingiza Carlos hospitalini.
A nurse takes Carlos into the hospital.
Mguu wa Carlos unauma sana na ana wasiwasi.
Carlos’s leg hurts a lot, and he is worried.
Madaktari wawili wanaupasua mguu wake.
Two doctors operate on his leg.
Wazazi wake wanamtembelea, wanaulizia jinsi ajali ilivyotokea.
His parents visit him. They ask him how the accident happened.
Wanampeleka nyumbani. Carlos anatumia magongo.
They drive him home. Carlos is using crutches.