Kip anataka kula tambi.
Kip feels like eating some noodles.
Kip anamuomba rafiki yake waende pamoja.
Kip asks a friend to join him.
Wanatafuta sehemu ya kula.
They look for a place to eat.
Wanaiona sehemu panapouzwa tambi.
They find somewhere that sells noodles.
Kip na rafiki yake wanatafuta meza.
Kip and his friend find a table.
Wanaketi chini na wanamwita mhudumu.
They sit down and call the waiter.
Mhudumu anakuja, Kip anaagiza tambi.
The waiter comes. Kip orders noodles.
Rafiki yake anaagiza tambi pia.
His friend orders noodles too.
Wote wanapata glasi ya maji.
They each get a glass of water.
Mhudumu analeta chakula.
The waiter brings the food.
Wanaongeza mchuzi na chumvi na wanakoroga tambi.
They add sauce and salt, and stir the noodles.
Kip na rafiki yake wanakula tambi. Ni tamu.
Kip and his friend eat the noodles. They are delicious.